DSpace Repository

Ubaadausasa kama kunga ya uandishi katika riwaya za dunia yao (2006) na nyuso za mwanamke (2010) Za S. A. Mohamed Na Unaitwa Nani? (2008) Ya K. W. Wamitila

Show simple item record

dc.contributor.author Muigai, Mary Njambi
dc.date.accessioned 2024-03-26T08:54:31Z
dc.date.available 2024-03-26T08:54:31Z
dc.date.issued 2024
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/8969
dc.description.abstract Riwaya za Kiswahili zilizoandikwa katika miaka ya hivi karibuni zinakaidi uandishi uliozoeleka wa kimapokeo uliopendekezwa na akina Aristotle, na kugeukia mtindo mpya wa uandishi wa kimajaribio wa kibaadausasa. Utafiti huu basi unachunguza uandishi wa kibaadausasa katika riwaya zilizoteuliwa za Kiswahili zilizoandikwa katika K21, yaani, Dunia Yao, Nyuso za Mwanamke na Unaitwa Nani? Riwaya hizi zina matumizi mengi ya uhalisia mazingaombwe ambayo huenda kinyume na kaida za uhalisia. Licha ya hayo, waandishi wa riwaya hizi hurejelea matini nyingine katika kazi zao zikiwemo za kifasihi, kidini, kisanaa, kihistoria, kifalsafa na kisaikolojia. Hata hivyo, uandishi huu mpya haujafanyiwa utafiti wa kutosha ili kuubainisha katika maandishi ya fasihi ya Kiswahili na kuonyesha athari zake kwa msomaji wa kazi hizi. Lengo la utafiti lilikuwa ni kubainisha na kuhakiki vipengele vya ubaadausasa katika riwaya zilizotafitiwa kama vile matumizi ya uchopekaji wa vipande vya simulizi, matumizi ya uhalisia mazingaombwe na matumizi ya mwingiliano matini. Utafiti huu uliegemea katika falsafa ya ubaadausasa na kuongozwa na nadharia ya ubaadausasa ambayo hupendekeza uanuwai wa mawazo kwa kukaidi kuwepo na mtazamo mmoja wa kueleza ulimwengu na tajriba za binadamu, au simulizi kuu. Usampuli wa kimaksudi ulitumika kupata data kwa kujikita katika riwaya zilizoandikwa katika K21 na ambazo zilidhihirisha vipengele vya ubaadausasa. Data ilikusanywa kupitia usomaji wa kina wa riwaya zilizoteuliwa kwa kuzingatia mihimili ya nadharia ya ubaadausasa iliyodhihirika kwa wingi katika riwaya hizo. Data ilichanganuliwa kwa kutumia mihimili ya nadharia ya ubaadausasa na kuwasilishwa kwa lugha ya nathari. Utafiti uligundua kuwa baadhi ya vipengele vya kibaadausasa vilitumiwa kimaksudi na waandishi ili kukaidi simulizi kuu zilizotawala. Riwaya za kibaadausasa zilitumia uchopekaji wa vipande vya simulizi kuvuruga urazini, mshikamano na muumano wa usimulizi wa riwaya za kimapokeo. Kimaudhui, riwaya hizi zinapuuza na kutilia shaka simulizi kuu inayohusiana na maana ya uhuru katika mataifa mengi ya Afrika kwa kusaili mwelekeo chanya uliohusishwa uhuru kuwa ungeleta maendeleo katika mataifa na badala yake kuonyesha hali ya utamauishi inayotawala mataifa haya. Riwaya hizi pia zinasaili hali ya utumwa miongoni mwa Waafrika wanaohamia ughaibuni kutafuta maisha bora humo kwa kuonyesha changamoto ambazo wahamiaji hupitia. Hali kadhalika, riwaya hizi zinafichua itikadi zilizofichika ndani ya misaada inayoletwa katika mataifa ya Afrika kutoka mataifa ya Ulaya na kuibainisha kama chambo cha kueneza ukoloni mamboleo kwa urahisi katika K21. Hali kadhalika, katika riwaya zilizotafitiwa mipaka kati ya uhalisia na umazingaombwe imezibwa kupitia matumizi ya wahusika na matukio ya ajabu kama vile mizuka, vivuli, wafu pamoja na wahusika wenye nguvu za kiajabu ili kuwakilisha hali halisi ya dunia ya sasa ambayo imejaa mambo mengine ya ajabu yasiyoelezeka. Fauka ya hayo, utafiti uligundua kuwa riwaya zilizoteuliwa zilitumia mwingiliano matini kwa wingi. Kutokana na matokeo ya utafiti huu, tunahitimisha kwa kusema kuwa mtindo wa uandishi wa ubaadausasa umetumika sio tu kama mbinu ya kiumbuji bali katika kudhihirisha fujo, ghasia na ukosefu wa mshikamano katika ulimwengu wa K21 kwa kukaidi simulizi za awali. Utafiti huu unatoa mchango katika taaluma ya usomi kwa kueleza vipengele vya ubaadausasa katika riwaya zilizoteuliwa za utafiti huu na namna ya kuzisoma kwa jumla. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Moi University en_US
dc.subject Ubaadausasa en_US
dc.subject Kunga en_US
dc.title Ubaadausasa kama kunga ya uandishi katika riwaya za dunia yao (2006) na nyuso za mwanamke (2010) Za S. A. Mohamed Na Unaitwa Nani? (2008) Ya K. W. Wamitila en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account