DSpace Repository

Kisiwa cha Migingo: diskosi tepetevu

Show simple item record

dc.contributor.author Obuchi, Samuel M.
dc.contributor.author Sangili, Nabeta K. N.
dc.date.accessioned 2023-11-02T07:49:44Z
dc.date.available 2023-11-02T07:49:44Z
dc.date.issued 2017
dc.identifier.uri https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/74
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/8293
dc.description.abstract Makala haya yanaangaza diskosi tepetevu kama inavyojitokeza katika lugha iliyotumiwa na viongozi mbalimbali wa Afrika Mashariki kuhusiana na umiliki wa kisiwa cha Migingo. Wandishi wanajadili matumizi ya lugha ya viongozi hawa, hususan Rais Yoweri Museveni ambaye alidai kwamba pasina shaka, kisiwa cha Migingo kipo chini ya himaya ya Kenya ila maji yanayokizunguka yanamilikiwa na Uganda. Baadhi ya viongozi kutoka Uganda walidai kwamba hapakuwa na sababu ya upande wa Kenya kung’ang’ania mwamba au jiwe lisilozidi kipimo cha uwanja wa mpira. Matamshi haya yalizua mjadala mrefu sana kuhusiana na umiliki wa kisiwa hiki huku pande mbili zinazohusika zikishikilia misimamo mikali ambayo, pasina shaka yoyote, ingesababisha kutoelewana na pengine, machafuko ya kisiasa. Katika makala haya, tunauangazia mgogoro huu ndani ya nadharia ya Diskosi Hakikifu Changanuzi (DHC). Katika kufanya hivi, tutajaribu kuonyesha namna mamlaka na nguvu za kisiasa na kijamii huongoza maingiliano yanayohusu mataifa yanayozozania kipande fulani cha ardhi.Van Dijk (1998) anafafanua Diskosi Hakikifu Changanuzi kama mtalaa unaoshughulikia uhakiki wa matini ama iliyoandikwa au inayosemwa, kwa lengo la kutambua vianzo vya mamlaka, utosawa, na amri juu ya upendelevu. DHC huchunguza namna hali mbalimbali za mamlaka huhifadhiwa na kuendelezwa katika miktadha mahususi ya kijamii, kisiasa na kihistoria. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher Mwangaa wa Lugha en_US
dc.subject Diskosi en_US
dc.subject Mgogoro en_US
dc.title Kisiwa cha Migingo: diskosi tepetevu en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account