DSpace Repository

Udhihirikaji wa mtafsiri katika muktadha wa baadaukoloni

Show simple item record

dc.contributor.author Magugu, Vincent N.
dc.contributor.author Oduori, Robert W.
dc.contributor.author Kandagor, Mosol
dc.date.accessioned 2023-11-02T06:06:00Z
dc.date.available 2023-11-02T06:06:00Z
dc.date.issued 2022
dc.identifier.uri https://www.royalliteglobal.com/african-languages/article/view/744
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/8280
dc.description.abstract Maendeleo katika taaluma ya tafsiri mwanzoni mwa miaka ya tisini yalibadilisha mtazamo kuhusu dhana ya tafsiri na kutambua upana na mabadiliko yake. Kupanuka kwa upeo wa taaluma hii kumeeleza na kuumba upya dhima ya mtafsiri. Nafasi ya mtafsiri imebadilika kutoka kwa daraja la kuvusha ujumbe pasi kuuathiri hadi kumtambua mtafsiri kuwa kiungo muhimu kinachoathiri mchakato na zao la tafsiri. Dhana kama vile ulinganifu, uaminifu pamoja na uhakiki wa ubora ambazo awali zilikuwa zenye umuhimu mkuu katika taaluma ya tafsiri zimesukumwa pembeni huku vipengele visivyokuwa vya kiisimu vikitiliwa mkazo. Ufasili na utafsiri wa matini ambao awali ulikuwa mchakato wa kiisimu na kimatini umebadilika na kujiegemeza zaidi kwa vipengele vya kitamaduni na vipengele nje ya isimu. Hali hii ni kweli tunapodhukuru tafsiri za fasihi katika muktadha wa baadaukoloni. Mtafsiri anadhihirika bayana kupitia kwa uteuzi wa kimakusudi ambao unajiegemeza kwa mikakati ya uibuaji ugeni hasa katika kushughulikia vipengele vinavyofungamana na utamaduni chanzi. Mikakati hii inaibua lugha mesto ambayo inahusiana kwa karibu na dhana ya utofauti wa kiisimu na kitamaduni katika mazingira ya baadaukoloni. Kwa kuchunguza tafsiri ya riwaya ya Caitaani Mutharaba-ini ya Ngugi wa Thiong’o kwa Kiingereza, Makala hii imejadili jinsi matini tafsiri imegeuzwa kuwa jukwaa la kukabiliana na ubabe wa kibepari katika ngazi ya isimu na utamaduni pamoja na jinsi udhihirikaji wa mtafsiri unavyobainika kupitia kwa kuchunguza uteuzi wa kimakusudi wa kiisimu ambao mtafsiri alifanya. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher Royallite publishers global en_US
dc.subject Uibuaji ugeni en_US
dc.subject Tafsiri za baadaukoloni en_US
dc.title Udhihirikaji wa mtafsiri katika muktadha wa baadaukoloni en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

Files Size Format View

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account