Moi University Open Access Repository

ukiushi katika tafsiri: uhakiki wa tamthilia nitaolewa nikipenda

Show simple item record

dc.contributor.author Kamotho John Njoroge
dc.date.accessioned 2018-03-07T10:18:03Z
dc.date.available 2018-03-07T10:18:03Z
dc.date.issued 2017-01-12
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/788
dc.description.abstract Utafiti huu umehusisha uchunguzi wa usuli wa sanaa ya tafsiri. Utafiti umechanganua kipengele cha ukiushi katika tamthilia Nitaolewa Nikipenda ambayo ni tafsiri ya Kiswahili ya tamthilia Ngaahika Ndeenda. Utafiti huu umefanya uchanganuzi linganishi wa lugha iliyotumiwa katika Matini Chanzi ya Ngaahika Ndeenda iliyo katika lugha ya Gĩkũyũ na Matini Tafsiri ya Nitaolewa Nikipenda iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. Utafiti umelenga kuchunguza Matini Tafsiri ilivyokiuka kutoka Matini Chanzi. Utafiti umechunguza zaidi dhana kuwa Matini Tafsiri ni ‘kivuli tu’ cha Matini Chanzi na hivyo kuihukumu kama kazi sahihi au isiyo sahihi. Utafiti huu umetumia Nadharia ya Mawasiliano katika Tafsiri ya Nida ambayo ni nguzo ya kanuni na michakato muhimu katika zoezi la tafsiri. Vitabu vya wataalamu mbalimbali vinavyohusu Nadharia ya Tafsiri na ukiushi katika tafsiri vimesomwa na mawazo yao kunakiliwa. Ngaahika Ndeenda na Nitaolewa Nikipenda vimesomwa kwa makini na kulinganishwa kwa mujibu wa lugha iliyotumiwa kwa kutumia maana kama kaida. Utafiti huu umechanganua ukiushi katika Tamthilia Tafsiri ya Nitaolewa Nikipenda na vilevile kujadili aina za ukiushi katika Tamthilia hii. Aidha umbuji kama kiungo cha ukiushi katika Matini Tafsiri ulitathminiwa. Tasnifu hii umejikita katika Nadharia ya Mawasiliano katika Tafsiri ya Nida ambayo husisitiza mawasiliano mwafaka kati ya Matini Tafsiri na Hadhira Pokezi. Utafiti umefanywa kwa kuchambua vitabu vya wananadharia wa tafsiri mbali na kuchanganua maneno ya Matini Tafsiri kwa kuyalinganisha na maneno ya Matini Chanzi. Sampuli za maneno, sentensi na vishazi vimetambuliwa na kunakililiwa kwa utaratibu, kuonyesha vilivyowakilishwa katika Matini Chanzi ya Gĩkũyũ na chini yake vilivyohawilishwa katika Matini Tafsiri ya Kiswahili. Maneno, vishazi na sentensi hizi zimechanganuliwa kiulinganishi halafu mahitimisho kufanywa. Uchanganuzi wa data iliyoshughulikiwa umethibitisha kuweko kwa ukiushi katika Matini Tafsiri. Ukiushi wowote uliopatikana katika Matini Tafsiri umeainishwa katika aina mbalimbali za ukiushi mathalani ukiushi wa kifonolojia, ukiushi wa kisintaksia na ukiushi wa kisemantiki. Athari ya maana ya ujumbe katika Matini Chanzi na Matini Pokezi imechunguzwa pia. Utafiti umezingatia dhima ya mtafsiri kama msanii na jinsi anavyokiuka maana iliyoko katika Matini Chanzi wakati anapotafsiri. Ni matumaini yangu kuwa utafiti huu utawafaa wanafunzi na wasomi ambao watatafitia mbinu za tafsiri katika kazi za kifasihi. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher MOI UNIVERSITY en_US
dc.subject NITAOLEWA NIKIPENDA en_US
dc.title ukiushi katika tafsiri: uhakiki wa tamthilia nitaolewa nikipenda en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account