Abstract:
Makala hii inatathmini shughuli za kiujasiriamali nchini Kenya kwa kutumia ‘Kiswahili’.
Shughuli zinazoangaziwa zinajikita katika maeneo mbalimbali ambamo aina fulani za
Kiswahili zinajitokeza kwa kuzingatia kwamba kuna “viswahili” vingi vinavyotumiwa
nchini Kenya. Neno viswahili katika muktadha huu linatumika kwa maana ya aina
mbalimbali za Kiswahili zisizo sanifu ambazo zinapatikana katika shughuli za kila siku
zinazoendeshwa na binadamu. Viswahili hivi hutokana na wazungumzaji kutoka
makabila na maeneo mbalimbali nchini Kenya wanaokitumia Kiswahili. Tumeendesha
mjadala unaojaribu kuonyesha jinsi gani ujasiriamali wa Kiswahili umechangia katika
kukua kwa Kiswahili katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini iliyopita. Mjadala huu
umeongozwa na dhana ya ujasiriamali kama inavyofasiriwa na taaluma ya uchumi kwa
kuiegemeza katika muktadha wa uchumi na lugha. Kwa hivyo, tumeangazia ujasiriamali
katika shughuli mbalimbali kama vile vyombo vya habari, biashara kupitia mabango na
uchapishaji. Isitoshe, tathmini imefanywa ili kudhihirisha athari chanya na hasi kisarufi
na kimawasiliano katika kukua kwa Kiswahili kutokana na matumizi yake kiujasiriamali
ili kufichua msambao wa athari hizo kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki