Abstract:
Makala haya yanaangazia chimbuko la “kalewenoik” yaani methali za Kinaandi na
uainishaji wa methali zenyewe huku yakijaribu kubainisha hadhira iliyotungiwa methali
hizo. Kwa mfano iwapo zilitungiwa watu maalum na iwapo zilisemwa wakati maalum.
Aidha, tumeshughulikia malengo ya methali katika jamii ya Kinandi pamoja na umuhimu
kwa wasemaji, wasemewa na jamii kwa jumla. Tumejaribu pia kutafsiri baadhi ya methali
hizi na kutolea maana na matumizi katika jamii husika. Hii ni kutokana na utafiti
uliofanyika katika Kaunti ya Nandi na Uasin Gishu ambapo tuliwasaili wazee 15 tofauti
wenye umri wa miaka 65 na zaidi.