Moi University Open Access Repository

Mabadiliko ya kimofofonemiki katika msamiati mkopo wa Kikipsigis

Show simple item record

dc.contributor.author Cherono, Naomi J.
dc.contributor.author Munyua, J. G.
dc.contributor.author Ogechi, Nathan O.
dc.date.accessioned 2023-07-21T08:10:09Z
dc.date.available 2023-07-21T08:10:09Z
dc.date.issued 2023
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/7853
dc.description.abstract Kila lugha ni mfumo huru unaojitosheleza kisarufi. Ingawa hivyo, wasemaji wa lugha tofauti wanapotagusana kimawasiliano, lugha zao huweza kuathiriana kisarufi, na athari mojawapo huwa ni ukopaji wa msamiati. Ni kutokana na hali hii ambapo utafiti huu ulichunguza kanuni zinazofuatwa katika uingizwaji wa msamiati mkopo wa Kiswahili na Kiingereza katika Kikipsigis. Makala hii ilichunguza mabadiliko ya kimofofonemiki yanayotokea katika msamiati mkopo unapoingizwa katika mfumo wa Kikipsigis. Vilevile, sababu za ukopaji zilibainishwa. Data ya utafiti iliteuliwa kimakusudi. Utafiti ulitambua kuwa Kikipsigis hufupisha irabu ndefu katika msamiati mkopo. Vilevile, irabu unganifu husahilishwa ili zikubalike katika Kikipsigis. Kimsingi tulitambua kuwa Kikipsigis hutohoa irabu ngeni kwa kutumia irabu asili zinazokaribiana kimatamshi. Ilibainika pia kwamba Kikipsigis hakiruhusu mfuatano wa konsonanti mwanzoni mwa neno. Kwa hivyo, Kikipsigis hutohoa msamiati wa aina hii kwa kuchopeka irabu. Katika kuchunguza vichocheo vya ukopaji, makala hii ilibainisha kwamba Kikipsigis hukopa msamiati ili kurejelea dhana ngeni isiyokuwepo katika utamaduni wake. Hata hivyo, uchanganuzi ulionyesha kuwa Kikipsigis wakati mwingine hukopa msamiati hata kama kina msamiati asilia kwa sababu ya ubadilishaji msimbo, msamiati mkopo ni sahili na rahisi kutamkwa ukilinganishwa na kisawe chake cha Kikipsigis. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.subject Msamiati mkopo en_US
dc.subject Utohozi en_US
dc.subject Mabadiliko ya kimofofonemiki en_US
dc.title Mabadiliko ya kimofofonemiki katika msamiati mkopo wa Kikipsigis en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account