Moi University Open Access Repository

Mwingilianomatini katika tenzi za fumo liyongo, ikidadi na mayasa, Gilgamesh na simulizi ya Samson

Show simple item record

dc.contributor.author Kiprotich, Priscah J
dc.date.accessioned 2023-01-17T07:20:24Z
dc.date.available 2023-01-17T07:20:24Z
dc.date.issued 2022
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/7195
dc.description.abstract Tenzi ni tungo za kale katika historia ya ushairi na Fasihi ya Kiswahili. Aidha, tenzi zinahusisha masimulizi marefu yaliyosukwa kihadithi na hushirikisha wahusika wanaojenga mfululizo wa matukio katika hadithi mahususi. Ingawa kazi zilizoteuliwa katika utafiti huu ziliandikwa katika vipindi tofauti kihistoria, mwangwi fulani unabainika. Utafiti huu ulitathmini vipi mwangwi huu unavyobainika katika matini teule. Tasnifu hii inahusu mwingilianomatini katika Tenzi za Fumo Liyongo (UFL), Mikidadi na Mayasa (UMM), Gilgamesh (UG) na Simulizi ya Samsoni (SS). Utafiti ulichunguza mwingiliano wa kimatini kwa kuzingatia vipengele vya mbinu ya usimulizi, sifa za wahusika na kikale cha safari ya shujaa katika kazi teule. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa ni: kufafanua mwingiliano wa mbinu ya kisimulizi katika UFL, UMM, UG na SS; kuonyesha mwingiliano wa sifa za wahusika wakuu katika matini teule na kuhakiki maingiliano ya kikale cha safari kama kigezo muhimu kinachodhihirika katika tenzi. Nadharia zilizoongoza utafiti huu ni Mwingilianomatini na Vikale. Mwasisi wa nadharia ya Mwingilianomatini ni Julia Kristeva (1980). Mwingilianomatini inasisitiza kuwa kazi za kifasihi huhusiana na kutegemeana ili kuzalisha maana upya. Nadharia hii ilitumika kuonyesha namna masuala ya mbinu ya usimulizi na sifa za wahusika wakuu zinavyoingiliana na kuathiriana katika matini teule. Aidha, nadharia ya Vikale ilitumika kuhakiki maingiliano ya kikale cha safari katika matini teule. Kwa mujibu wa Campbell (2008), nadharia hii inasisitiza kuwa vikale ni ishara bia zilizoenea hivyo kutambulika katika kazi za kisanii. Inaeleza hatua za safari ya shujaa inayopatikana katika jamii mbalimbali. Nadharia hii ilirejelewa katika uchanganuzi wa hatua mbalimbali za motifu ya safari ya shujaa. Mbinu ya uteuzi wa kimaksudi ilitumika ili kuteua sampuli na kupata data iliyokidhi mahitaji ya utafiti huu. Matini zilizoteuliwa ni: Simulizi ya Samsoni kutoka katika Biblia Takatifu, kitabu cha Waamuzi, sura ya kumi na tatu hadi kumi na sita, Utendi wa Fumo Liyongo uliotungwa na Mohammed Kijumwa kama anavyoeleza Mulokozi (1999), Utendi wa Mikidadi na Mayasa kama unavyoelezwa na Bashir (1972). Aidha, Simulizi ya Gilgamesh ilirejelewa kutoka Utendi wa Gilgamesh, tafsiri ya Kiingereza ya Kovacs (1998). Utafiti huu ni wa maktabani. Kuhusu ukusanyaji wa data, mbinu ya uchambuzi wa yaliyomo ilitumika. Data ilikusanywa kwa kusoma na kuchuja taarifa muhimu katika matini teule zilizoakisi mada ya utafiti huu. Uchanganuzi wa data ulifanywa kulingana na malengo ya utafiti na mihimili ya nadharia za mwingilianomatini na vikale. Uwasilishaji wa matokeo ya data ni wa kimaelezo katika sura mbalimbali. Lengo la kwanza la utafiti huu lilionyesha ulinganifu katika kazi teule zinazodhihirisha mtiririko wa matukio ya kiajabu kwa kutumia mbinu ya usimulizi wa ki-utendi, usimulizi wa nafsi ya kwanza, usimulizi wa nafsi ya tatu na vipengele katika matumizi ya lugha. Kwenye lengo la pili, utafiti ulibainisha kuwa licha ya tofauti za kiusuli, hulka na sifa za wahusika wakuu zinaingiliana katika vipengele vya sifa za ukatili, uongozi, ushujaa, majigambo, tanzia na athari ya mwanamke kama mhusika katika maisha ya wahusika wakuu katika UFL, UMM, UG na SS. Katika lengo la tatu, utafiti umebainisha maingiliano katika motifu ya safari ya shujaa inavyodhihirika katika kazi teule. Utafiti umeonyesha kuwa Biblia Takatifu inaweza kutumika kama matini rejea katika uchambuzi wa kazi za fasihi. Matokeo ya utafiti huu yanafaa kwa wanafunzi, walimu na wapenzi wa fasihi. Inabainika kuwa UFL, UMM, UG na SS ni tungo za kale, hivyo utafiti huu unatoa fursa ya kuziangalia kazi hizi upya kwa lengo la kukipa kizazi cha Karne ya Ishirini na Moja mafunzo yanayopatikana katika kazi za kijadi. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Moi University en_US
dc.subject Ushairi en_US
dc.subject Fasihi en_US
dc.title Mwingilianomatini katika tenzi za fumo liyongo, ikidadi na mayasa, Gilgamesh na simulizi ya Samson en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account