Moi University Open Access Repository

Kiswahili na Teknolojia ya habari na mawasiliano katika huduma za Afya nchini Kenya

Show simple item record

dc.contributor.author Mawunyo Adzo, Forfoe
dc.date.accessioned 2022-12-02T07:45:23Z
dc.date.available 2022-12-02T07:45:23Z
dc.date.issued 2022
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/7148
dc.description.abstract Azma ya kutumia mifumo ya kielektroniki katika huduma za afya, inayojulikana kama huduma za afya kielekroniki, ni kuboresha kiwango na upatikanaji wa huduma za afya kwa wagonjwa. Aina mojawapo ya huduma za afya kielektroniki ni programu za afya za rununu ambayo kwayo wagonjwa wanaweza kupokea huduma za afya kupitia simu za rununu kwa usaidizi wa programu za mtandao. Kenya imeshuhudia ukuaji mkubwa wa mpenyo wa kiteknolojia katika utoaji wa huduma za afya na ukuaji huu umeibua suala la uteuzi na matumizi ya lugha za kiasili katika programu hizi za kielektroniki. Kuambatana na haya, utafiti huu ulilenga kuchunguza nafasi na kiwango cha ukubalikaji wa matumizi ya Kiswahili katika muktadha wa huduma za afya kielektroniki nchini Kenya. Kwa hivyo, azma ya utafiti huu ilikuwa ni kutathmnini upatikanaji na mpenyo wa Kiswahili katika huduma za afya kielektroniki kwa kuzingatia madhumuni matatu: kubainisha aina za mifumo ya huduma za afya kielektroniki zipatikanazo nchini Kenya; kutathmini matumizi ya Kiswahili katika mifumo ya huduma za afya iliyokwisha bainishwa; na, kutathmini utayari wa watumiaji wa mifumo ya huduma za afya kielektroniki kukitumia Kiswahili. Ili kushughulikia vipengele vya kiteknolojia na kiisimu katika utafiti huu, nadharia mbili zilitumika. Nazo ni: Nadharia ya Lugha za Mtandao na Nadharia ya Ukubalifu wa Teknolojia. Nadharia ya Lugha za Mtandao ilisaidia kuchambua na kuelezea vipengele vya kiisimu jamii kuhusu matumizi ya Kiswahili katika huduma za afya kielektroniki. Aidha, nadharia hiyo ilituwezesha kutathmini athari za teknolojia kwa Kiswahili, kwa upande mmoja, na athari za Kiswahili kwa teknolojia, kwa upande mwingine. Nadharia ya Ukubalifu wa Teknolojia ilitumika kutathmini urahisi wa matumizi pamoja na manufaa-tarajiwa ya kukitumia Kiswahili katika dhana ya huduma za afya kielektroniki. Utafiti elezi ulitumika na kwa kutumia mkabala wa mbinu-mseto uliojumuisha njia za utafiti kitakwimu na zisizo za kitakwimu, data zilikusanywa kwa njia tatu: dodoso, uchambuzi wa nyaraka na mahojiana. Data zilizotokana na dodoso zilikusanywa kutika maeneo matatu nchini Kenya kwa kutumia dodoso iliyosambazwa na kujazwa kimtandao. Madaktari wanne walihojiwa katika hospitali mbalimbali mjini Eldoret ilhali data za uchanganuzi wa nyaraka zilitokana na programu 21 za huduma za afya kielektroniki zipatikanzo nchini Kenya. Usimbaji kidhamia ulitumika kuchanganua data za kitakwimu na takwimu elezi zilitumika kuchanganua data zisizo za kitakwimu na matokeo yakawasilishwa kwa michoro, majedwali na vielelezo. Ufasiri na mjadala kuhusu data vilionyesha kwamba programu za kiafya za rununu hupatikana na kutumiwa nchini Kenya. Hata hivyo, kiwango cha upatikanaji wa Kiswahili kwa jumla katika programu hizi ni 42.9% ilhali upatikanaji wa maandishi kwa Kiswahili ni 9.5%. Uchunguzi huu pia ulidhihirisha kwamba ingawa wahudumu wa afya na wagonjwa huenda wangependelea kutumia Kiswahili katika kushauriana, kuna uhaba wa ufahamu kuhusu uwepo wa istilahi za kiteknolojia zinazorejelea masuala ya afya kwa Kiswahili. Kwa sababu hiyo, Kiingerezakiliteuliwa na kutumiwa katika miktadha ya mashauriano na utambuzi wa kimatibabu. Utafiti huu ulihitimishwa kuwa, kwa sasa, Kiswahili si lugha ya msingi yanayotumika katika programu za kiafya za rununu nchini Kenya. Utafiti unapendekeza kwamba programu zilizopo za programu za kiafya za rununu zinafaa kutiwa msasa ili kujumuisha Kiswahili kama mojawapo ya lugha za kuteuliwa mteja anapofungua programu hizi. Pia utafiti unatoa wito wa kupitia tena na kutekeleza pendekezo la kufundisha Kiswahili kama somo la lazima kwa taaluma zote za vyuo vikuu nchini Kenya mintarafu ya ripoti ya Tume ya Mackay ya 1981. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher Moi University en_US
dc.subject Kiswahili en_US
dc.subject Teknolojia en_US
dc.subject Huduma za Afya en_US
dc.subject Programu en_US
dc.title Kiswahili na Teknolojia ya habari na mawasiliano katika huduma za Afya nchini Kenya en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account