Moi University Open Access Repository

Mwingilianotanzu na uchimuzi wa maudhui katika fasihi bunilizi za watoto

Show simple item record

dc.contributor.author Kirui, Cherono C.
dc.date.accessioned 2022-09-28T12:38:17Z
dc.date.available 2022-09-28T12:38:17Z
dc.date.issued 2022
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/6810
dc.description.abstract Japo bunilizi nyingi za watoto katika fasihi ya Kiswahili zinabainisha sifa za mwingilianotanzu kiumbo, hakuna utafiti ambao umeangazia suala hili. Utafiti huu unachunguza namna mwingilianotanzu unachimuza maudhui katika fasihi bunilizi za watoto. Malengo ya utafiti huu ni mosi; kupambanua namna tanzu mahsusi zinajenga bunilizi teule za watoto. Pili, kuchanganua namna tanzu mahususi zinachimuza maudhui katika bunilizi teule za watoto na tatu ni kuhakiki uamilifu wa maudhui kwenye tanzu husika kwa mtoto Mwafrika katika mazingira yake. Ili kutimiza malengo haya, utafiti uliongozwa na maswali yafuatayo: Kwanza, ni tanzu zipi zinazojenga fasihi bunilizi za watoto wa daraja la tatu? Pili, ni kwa namna gani vipengele vya mwingilianotanzu vinachimuza maudhui katika fasihi bunilizi teule za watoto? Mwisho, tanzu na maudhui yanayowasilishwa kwa bunilizi teule yana uamilifu upi kwa mtoto Mwafrika? Utafiti huu umejikita katika vitabu teule vya watoto; Mchezo wa Mtelezo na Hadithi Nyingine (Nandwa, 2016), Kade na Katana (Syokau, 2018), Mchezo wa Kobole (Momanyi, 2019), Kito Apepeta (Nandwa, 2013), Sitaki Iwe Siri (Matundura, 2008), Hidaya (Namlola, 2019), na Msiba wa Kujitakia (Kea, 2013). Nadharia ya Mwingilianomatini yake Kristeva (1960) na Nadharia ya Uoniafrika ya Asante (1980) ndizo kiunzi cha utafiti huu. Kristeva (1960) anadai kuwa matini siku zote huingiliana na kutegemeana. Ni kwa msingi huu ndipo utafiti huu unachunguza namna tanzu anuwai zinaingiliana na kuchimuza maudhui katika bunilizi teule za watoto. Kwa upande mwingine, Uoniafrika unasisitiza kuwa maisha ya Mwafrika lazima yatathminiwe kwa kuzingatia mwonoulimwengu wake. Nadharia hii ilituongoza kuhakiki namna tanzu zinazoingiliana katika bunilizi teule zinamwangazia mtoto Mwafrika katika mazingira yake. Ukusanyaji wa data ya kimsingi ulitokana na bunilizi saba za watoto. Sampuli ya kimakusudi ilitumiwa kuteua bunilizi hizo. Data ilichanganuliwa kiufafanuzi kulingana na maswali ya utafiti na mihimili ya nadharia za utafiti. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa mwingilianotanzu ni mojawapo ya mbinu ya kisanaa inayochimuza maudhui kama vile umaskini, dini, uzalendo, utangamano na mengine katika bunilizi teule. Utafiti huu ni kichocheo kwa wahakiki wa fasihi ya Kiswahili kuchunguza namna mwingilianotanzu unachimuza maudhui katika tanzu nyinginezo za fasihi andishi na simulizi. Aidha, utafiti huu unachangia pakubwa katika kubainisha vigezo vya utunzi hasa wa fasihi ya watoto katika Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika. en_US
dc.publisher Moi University en_US
dc.subject Bunilizi en_US
dc.title Mwingilianotanzu na uchimuzi wa maudhui katika fasihi bunilizi za watoto en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account