Moi University Open Access Repository

Lugha ya kiswahili katika Tamasha za Drama nchini Kenya: Kustawi au kudumaa?

Show simple item record

dc.contributor.author Waititu, Francis G
dc.date.accessioned 2022-01-17T10:01:37Z
dc.date.available 2022-01-17T10:01:37Z
dc.date.issued 2015-10
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/5683
dc.description.abstract Tamasha za drama ambazo hufanywa kila mwaka nchini Kenya ni mojawapo ya nyenzo zilizowekwa na wizara ya Elimu nchini kutoa elimu kwa vijana. Tamasha hizi ambazo zinajumuisha wanafuzi kutoka shule za malezi, msingi, sekondari, vyuo anuai na vyuo vikuu hufanyika kila mwaka. Tamasha huanzia mashinani na kilele huwa kujumuika kwa timu ambazo zimeshinda katika ngazi mbalimbali kwa mashindano ya kitaifa ambayo aghalabu hufanyika mwezi wa Aprili. Mojawapo ya malengo ya tamasha hizi ni ustawishaji wa lugha za Wakenya miongoni mwa wanaoshiriki. Tanzu mbalimbali kama michezo ya kuigiza, ngoma, mashairi, sarakasi na masimulizi huwasilishwa. Washiriki huwa na uhuru wa kuwasilisha chochote wanachokiwasilisha kwa lugha yoyote kuanzia Kiswahili, Kiingereza na lugha nyingine za Kenya. Hata hivyo, imebainika kuwa kazi nyingi ambazo hupata matuzo ni kazi katika lugha ya Kingereza. Makala hii inalenga kuchunguza kiwango cha matumizi ya lugha ya Kiswahili katika tanzu zinazowasilishwa hasa katika ngazi ya kitaifa. Makala itachunguza tanzu zinazowasilishwa kwa lugha ya Kiswahili huku ikilinganisha zinazowasilishwa kwa lugha ya nyingine ili kubainisha ni kwa nini tanzu kwa lugha ya Kiswahili hazifikii kupata matuzo. Aidha, makala itachunguza iwapo katika tamasha hizi, Kiswahili hupata nafasi ya kustawi au kudumaa. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Moi University en_US
dc.subject Tamasha en_US
dc.subject Drama en_US
dc.subject kudumaa en_US
dc.subject Kustawi en_US
dc.title Lugha ya kiswahili katika Tamasha za Drama nchini Kenya: Kustawi au kudumaa? en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account