DSpace Repository

Changamoto za tafsiri katika enzi ya utandawazi

Show simple item record

dc.contributor.author Toboso, Mahero
dc.contributor.author Kandagor, Mosol
dc.date.accessioned 2021-05-12T10:14:10Z
dc.date.available 2021-05-12T10:14:10Z
dc.date.issued 2021-04-21
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/4436
dc.description.abstract Ulimwengu unaendelea kuwa mdogo kwa sababu ya utandawazi. Katika muktadha wa lugha na fasihi ya Kiswahili, tunaweza kusema kuwa utandawazi umekuwa na athari kubwa kifasihi, kiisimu na kijamii. Ulimwengu wa sasa umeshuhudia ongezeko la matumizi mapana ya lugha anuwai za ulimwengu mbali na Kiingereza. Lugha kama Kiswahili, Kihindi, Kimandarin, Kichina, Kirusi, Kifaransa, Kiarabu na Kijapani zimeshuhudia ongezeko la matumizi yake kutokana na utandawazi. Kwa sababu hii, wafasiri na wakalimani walio na ujuzi katika lugha hizi wanahitajika katika maeneo anuwai ya ulimwengu. Hii ni kusema kuwa utandawazi umesababisha kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za tafsiri. Mbali na kupanuka kwa matumizi ya lugha, mahitaji haya pia yamesababishwa na teknolojia mpya ambayo imesababisha kupungua kwa gharama ya kubadilishana kwa ujumbe na matokeo ya tafiti. Changamoto za kisiasa ulimwenguni nazo zimesababisha haja ya kuwapo kwa wafasiri na wakalimani wengi katika kila pembe ya ulimwengu ili kushirikishwa katika michakato ya kutafuta amani na mapatano. Kwa sababu hii, changamoto anuwai zimezuka na kukumba wafasiri ikiwamo michakato ya tafsiri na vifaa vinavyotumika kutekeleza jukumu hili. Makala haya yanajadili changamoto zinazowakumba wafasiri katika michakato yao ya kutafsiri matini mbalimbali enzi au zama za sasa, zama za utandawazi. en_US
dc.publisher mulika en_US
dc.subject utandawazi en_US
dc.subject lugha en_US
dc.subject fasihi en_US
dc.title Changamoto za tafsiri katika enzi ya utandawazi en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account