DSpace Repository

Jinsi vipengele vya kitamaduni katika matini teule ya kiswahili na kikalenjin vilivyochangia mtafsiri kuiandika upya Bukuit ne tilil.

Show simple item record

dc.contributor.author Kandagor, Mosol
dc.contributor.author Jepkoech Singoei, Jane
dc.contributor.author Mwanakombo, Mohamed
dc.date.accessioned 2021-05-12T07:45:14Z
dc.date.available 2021-05-12T07:45:14Z
dc.date.issued 2020-09-30
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/4434
dc.description.abstract Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza jinsi vipengele vya kitamaduni katika matini teule ya Kiswahili na Kikalenjin vilivyochangia mtafsiri kuiandika upya Bukuit ne Tilil. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ambazo ni nadharia ya tafsiri vitendo ambayo ilitumika kubaini jinsi tofauti za kimazingira kati ya hadhira ya matini asilia na ya matini pokezi ilivyopelekea uandishi upya kufanyika wakati wa kutafsiri. Nadharia ya pili ni ya ulinganifu, ambapo matini asilia ililinganishwa na matini pokezi ili kubaini kama ujumbe ulihifadhiwa katika matini tafsiri. Aidha, tamaduni, matumizi ya msamiati na sarufi zililinganishwa kwa kuchunguza mikakati na mbinu zilizotumika kutafsiri matini asilia, na hivyo kubaini uandishi upya katika matini pokezi. Data zilikusanywa kupitia uchunguzi maktabani na vilevile kuwasaili washikadau katika Ofisi ya Utafsiri wa Bibilia ya Kapsabet na Shirika la Kutafsiri Biblia nchini, pamoja na wazungumza lugha ya Kikalenjin ambao walituelekeza juu ya matumizi ya baadhi ya maneno. Usampuli wa kimakusudi ulitumiwa ili kupata data iliyotumika katika uchanganuzi. Kitabu cha Mithali katika Agano la Kale kiliteuliwa kwa minajili ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa: utamaduni wa Waswahili na wa Wakalenjin ni tofauti na hii ilipelekea uandishi upya ufanywe katika tafsiri. Utafiti unapendekeza yafuatayo: Sera za elimu kuhusu lugha za kienyeji zinafaa kutilia maanani tafsiri ya matini za kufundishia. en_US
dc.publisher Consortium Publishing en_US
dc.subject kitamaduni en_US
dc.subject matini en_US
dc.subject mtafsiri en_US
dc.subject Bukuit ne Tilil en_US
dc.title Jinsi vipengele vya kitamaduni katika matini teule ya kiswahili na kikalenjin vilivyochangia mtafsiri kuiandika upya Bukuit ne tilil. en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account