Show simple item record

dc.contributor.author Kandagor, Mosol
dc.date.accessioned 2020-12-07T06:42:14Z
dc.date.available 2020-12-07T06:42:14Z
dc.date.issued 2019
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/3725
dc.description.abstract Toleo hili linajumuisha jumla ya makala ambayo yanatanda katika taaluma mbalimbali za lugha na fasihi. Makala ya Tirus Mutwiri Gichuru, Kitula King’ei na Ireri Mbaabu yamebainisha kuwa maarifa na tajriba zilizofichamwa kwenye utambuzi huwa nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko ya maana za leksia. Imebainika wazi kuwa muundo wa maana na maumbile ya mwanadamu hasa hisia zake tano na ufasili wake wa ulimwengu husaidia mwanadamu kukabiliana na dhana mpya zinazoibuka katika mazingira halisi na ya kidhahania. Nao Amiri Swaleh and Rayya Timammy wamechambua utendi wa Mtu ni Utu (1978) uliotungwa na Ahmad Nassir Juma Bhalo. Waandishi wameangazia mafunzo makuu yanayojitokeza katika utendi huu; mafunzo ambayo yanakuza maadili ya kijamii. Uchambuzi huu umeegemea misingi ya Dini ya Kiislamu, kulingana na tajriba na maarifa ya mtunzi wa utendi huu. Makala ya Gakuo J. Kariuki yanaangazia baadhi ya changamoto zinazokumba taaluma ya ufasiri, uelewekaji na ufundishaji wa somo la ushairi katika shule za sekondari nchini Kenya. Mawazo na kauli zinazoshereheshewa katika makala haya zinazotokana na utafiti wa kisayansi uliofanywa katika kaunti mbili za Mombasa na Trans Nzoia. Rufus Karani Munyua, P. I. Iribemwangi na Tom M. Olali wameshughulikia suala la utafsiri kwa kudai kwamba chochote kinachoweza kusemwa katika lugha moja kinaweza pia kusemwa katika lugha nyingine. Waandishi hawa wamewarejelea wataalamu waliotukuka katika taaluma ya tafsiri kama vile Catford, Nida na Newmark kuhusiana na masuala wanayoyaibua. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher Moi University Press en_US
dc.subject Lugha en_US
dc.title Mwanga wa Lugha en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account