Moi University Open Access Repository

Uchanganuzi wa upole katika mazungumzo ya vipindi vya Sobetab Kapchi katika idhaa ya KASS FM

Show simple item record

dc.contributor.author Ngisirei Muge Tecla C.
dc.date.accessioned 2018-12-03T09:54:49Z
dc.date.available 2018-12-03T09:54:49Z
dc.date.issued 2018-11
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/2346
dc.description.abstract Utafiti huu ulilenga kushughulikia umuhimu wa upole katika mazungumzo kwa kuchanganua mikakati ya upole inayotumika katika vipindi vya Sobetab Kapchi (Maisha ya Jamii) kwenye idhaa ya KASS FM. Ili kutekeleza jukumu hilo, utafiti uliongozwa na madhumuni yafuatayo: kuchanganua mikakati ya upole inayotumika kuwasilisha vipindi vya Sobetap Kapchi (SK) katika idhaa ya KASS FM, kuhakiki athari za uzingatiaji na ukiukaji wa kanuni za upole kwenye vipindi vya SK, kutathmini hali zinazoathiri uteuzi wa mikakati ya upole katika vipindi husika vya SK na kupambanua na kujadili changamoto zinazosawiriwa na wahusika wa mazungumzo ya SK wakati wa utekelezaji wa kanuni za upole. Aidha, utafiti uliongozwa na maswali manne. Kwanza, je, ni mikakati gani ya upole inatumika kuendeleza mazungumzo ya SK kwenye idhaa ya KASS FM? Pili, uzingatiaji au ukiukaji wa mikakati ya upole una athari gani kwa mazungumzo ya vipindi vya SK? Tatu, Ni hali zipi zinaathiri uteuzi wa mikakati ya upole katika mazungumzo ya vipindi vya SK kwenye idhaa ya KASS FM? Mwisho, wahusika wa mazungumzo ya SK wanasawiri changamoto zipi wakati wa kutekeleza mikakati ya upole? Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Upole, hasa mhimili wa ‘kuokoa uso’, kama ilivyopendekezwa na Brown na Levinson. Kulingana na waasisi wa nadharia hii, uso ni thamani ya kijamii ambayo mtu hujipa kulingana na atakavyo kuchukuliwa na wengine. Unarejelea kile ambacho mtu anatamani katika mawasiliano yoyote. Nadharia ya Upole inaeleza kuwa mtu ana aina mbili za uso; uso chanya na uso hasi. Aidha, nadharia hii inasisitiza kuwa mawasiliano yoyote hufanikiwa iwapo washiriki wa mazungumzo wanazingatia kanuni za upole kwa makusudi ya kuokoa nyuso zao na za wenzao. Isitoshe, kila mshiriki wa mazungumzo anatakiwa kuhisi kukubalika na kupewa uhuru wa kutoingiliwa. Sampuli ya utafiti iliteuliwa kimakusudi kuambatana na nadharia ya utafiti, malengo na maswali ya utafiti pamoja na upeo wa utafiti kwa kuangazia masuala mahsusi ya kipindi hiki kulingana na utamaduni wa jamii ya Kikalenjin. ‘Pasta’ Edward Rotich na mwelekezi wa vipindi Winny Jepkorir (‘Koriryo’), ni wahusika wakuu na pamoja nao ni mashabiki waliochangia katika vipindi husika. Vipindi vya SK vilisikilizwa kwa makini kabla ya kunaswa. Kinasa sauti kilitumika kukusanya data kwa kurekodi vipindi vinane vya SK. Mwisho, hoja zinazohusiana na upole zilinakiliwa na kuwekwa kwenye makundi manne ya mikakati ya upole ili kuchanganuliwa. Makundi hayo ni ya mkakati wa kuwa kwenye rekodi, mkakati wa upole chanya, mkakati wa upole hasi na mkakati wa kuwa nje ya rekodi. Uchanganuzi wa data ulifanywa kimaelezo kwa kutumia mazungumzo ya washiriki kama mifano halisi. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa wahusika wa mazungumzo ya SK hutumia mikakati anuwai ya upole kuwasiliana ili kudumisha mahusiano kati yao. Pia, wahusika hao hukumbana na changamoto nyingi wanapotekeleza mikakati ya upole wakati wa mazungumzo. Kutokana na matokeo hayo, utafiti huu ni matini muhimu katika uwanja wa mawasiliano kwenye vyombo vya habari hasa vya redio.Utafiti huu ni mchango mkubwa kwa taaluma ya isimu, hasa kwa wale walimu na wanafunzi wa uamali na isimu-jamii, wanaotafitia suala la upole katika mazungumzo kwenye vyombo vya habari katika lugha yoyote ya Kiafrika, hasa lahaja za Kikalenjin. Pendekezo la jumla ni kuwa watafiti wajitokeze kushughulikia masuala ya upole katika nyanja za fasihi na tafsiri. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Moi University en_US
dc.subject KASS FM en_US
dc.subject Upole en_US
dc.subject Radio en_US
dc.title Uchanganuzi wa upole katika mazungumzo ya vipindi vya Sobetab Kapchi katika idhaa ya KASS FM en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account