Please use this identifier to cite or link to this item:
http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/9398
Title: | Mwelekeo wa kiubwege katika tamthilia ya kiswahili mintarafu ya Amezidi na Beluwa |
Authors: | Achieng, Vivian Odhiambo |
Keywords: | Kiubwege Tamthilia |
Issue Date: | 2024 |
Publisher: | Moi University |
Abstract: | IKISIRI Utafiti huu umeshughulikia mwelekeo wa kiubwege katika tamthilia ya Kiswahili, mintarafu ya Amezidi (1995) na Beluwa (2012). Nadharia iliyoongoza kazi hii ni nadharia ya Ubwege iliyoasisiwa na Albert Camus ambayo, kimsingi imeangazia ukosefu wa maana ya maisha ya binadamu ulimweguni. Data za uchunguzi huu zilitokana na uhakiki wa kazi hizi mbili kwa misingi ya mihimili ya nadharia ya ubwege. Madhumuni ya utafiti huu ni pamoja na; kuchunguza vipengele vya kiubwege kimaudhui na kifani katika tamthilia ya Amezidi na Beluwa, kujadili mwelekeo wa kiubwege katika tamthilia ya Amezidi na Beluwa pamoja na kutathmini mwelekeo wa kiubwege katika The Myth of Sisyphus. Kutokana na madhumuni haya, utafiti huu umejiegemeza kwenye nadharia tete kwamba Beluwa na Amezidi ni tamthilia za kiubwege, kuna kufanana kwa mwelekeo wa kiubwege katika tamthilia ya Amezidi na Beluwa na Albert Camus aliweka msingi wa nadharia ya Ubwege katika The Myth of Sisyphus . Tofauti na tafiti zilizofanywa hapo awali, utafiti huu umejikita katika mwelekeo wa kinadharia ambao wahakiki wengi hawakuzingatia katika tamthilia ya Amezidi. Aidha, utafiti huu umehusisha ulinganifu kinadharia ambao haukuchunguzwa na wahakiki wa awali. Huu ni utafiti wa kiuhakiki, na hivyo mbinu zilizotumiwa kukusanya data ni utafiti maktabani ambapo usomaji makinifu wa tamthilia hizi mbili ulichangia katika kudondoa vipengele vya kiubwege kama vinavyojitokeza katika tamthilia hizi mbili, na kudhihirisha mwelekeo wa kiubwege wa watunzi hawa pamoja na kubainisha mwelekeo wa kiubwege katika The Myth of Sisyphus (1942). Maktaba tuliyotumia ni ya Margaret Thatcher ya Chuo kikuu cha Moi, ambamo tulisoma majarida, vitabu na makala zinazohusiana na mada ya utafiti. Kadhalika tulitembelea tovuti mbalimbali zinazozungumzia Ubwege pamoja na kupakua makala mbalimbali yanayohusu ubwege. Mbinu ya kitaamuli ilitumika katika uchanganuzi wa data tuliyokusanya na kueleza matokeo ya utafiti. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kwamba tamthilia ya Amezidi na Beluwa ni kazi za kiubwege na watunzi walifuata mwelekeo wa kiubwege wake Albert Camus; ambaye anashikilia kwamba Mungu yupo japo binadamu hapaswi kuishi kwa matumaini ya kukombolewa naye bali, afanye juhudi za kujipatia maana ya maisha yake akisubiri kifo-ambacho ndicho hatima ya binadamu wa kiubwege. Mbali na utafiti huu kuweka wazi mwelekeo wa kiubwege wa Albert Camus katika The Myth of Sisyphus (1942), utaongeza maarifa yaliyopo kuhusu tamthilia za kiubwege na fasihi kwa jumla. |
URI: | http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/9398 |
Appears in Collections: | School of Arts and Social Sciences |
Files in This Item:
File | Description | Size | Format | |
---|---|---|---|---|
ACHIENG VIVIAN - MA 2024.pdf | 887.05 kB | Adobe PDF | View/Open |
Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.