Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/8316
Title: Kiswahili na lugha nyingine za kiafrika katika muktadha wa utandawazi
Authors: Obuchi, Samuel Moseti
Ochoi, Phillip F. O.
Keywords: Lugha
Utandawazi
Issue Date: 2017
Abstract: Makala haya yanatalii masuala mbalimbali yanayohusu Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika katika ulimwengu na malimwengu ya utandawazi. Kwa muda mrefu, wataalamu wengi wa masuala ya lugha na isimu wamekuwa mbioni katika kuuangazia uhusiano uliopo au unaopaswa kuwepo baina ya lugha na shughuli za kimsingi na maendeleo ya jamii. Mjadala huu hasa umekitwa kwenye mawazo na mikabala ambayo inahusiana moja kwa moja na nguvu na taratibu za utandawazi, ambapo inaaminika kwamba lugha zozote zile ambazo hazitumiwi katika shughuli na harakati za uzalishaji mali huenda zikamezwa na kusahauliwa kabisa hivi karibuni na utamaduni wa Kimagharibi ambao unajitokeza waziwazi katika harakati anuwai za kijamii kama vile uchumi, elimu, uvumbuzi na ugunduzi wa sayansi na teknolojia. Makala haya basi yanaonyesha namna Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika zinaweza kulindwa na kuhifadhiwa ili ziendelee kutumiwa na walio wengi katika shughuli zao za kila siku.
URI: https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/58/50
http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/8316
Appears in Collections:School of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
There are no files associated with this item.


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.