Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/8310
Title: Mwingiliano wa Kisimulizi katika Tenzi za 'Fumo Liyongo' (UFL), 'Gilgamesh' (UG), 'Mikidadi na Mayasa' (UMM) pamoja na 'Simulizi ya Samsoni' (SS)
Authors: Obuchi, Samuel M.
Kiprotich, Priscah J.
Mwanakombo, Mohamed
Keywords: Mwingilianomatini
Usimulizi
Issue Date: 2021
Publisher: Mwanga wa Lugha
Abstract: Makala haya yanajadili suala la mwingilianomatini katika tendi teule na matini ya kidini. Mabadiliko katika jamii yanayoletwa na teknolojia ya kisasa yamesababisha baadhi ya kazi za kijadi kama vile tenzi, kusahaulika. Tenzi ni hifadhi muhimu ya historia ya jamii, hivyo zinafaa kuhifadhiwa kwa kufanyiwa utafiti zaidi ili ziendelee kuwa na manufaa katika jamii. Kutokana na udurusu wa maandishi uliofanywa na watafiti, ilidhihirika kwamba tenzi za Fumo Liyongo (UFL), Gilgamesh (UG), Mikidadi na Mayasa (UMM) pamoja na Simulizi ya Samsoni (SS) zinawasilisha visa mbalimbali kwa njia ya usimulizi. Matini hizi teule zina mwangwi fulani unaohisika kisimulizi. Makala haya yamezingatia Biblia kama matini muhimu ambayo ina wingi wa kazi za kifasihi zinazohitaji kuhakikiwa, mojawapo ikiwa Simulizi ya Samsoni. Makala haya yamejadili mbinu za kisanii zilizotumika kisimulizi ili kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa.
URI: https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/199
http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/8310
Appears in Collections:School of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
There are no files associated with this item.


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.