Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/8286
Title: Uteuzi wa lugha katika mahubiri ya kikristo jijini Nairobi
Authors: Kevogo, Alex Umbima
Kandagor, Mosol
Keywords: Mahubiri
Muktadha
Issue Date: 2021
Publisher: Mwangaa wa Lugha
Abstract: Makala haya yalichunguza hoja zilizoathiri uteuzi wa lugha iliyotumiwa na wahubiri wa Kikristo jijini Nairobi katika mahubiri yao. Wahubiri kadha kutoka kwa makanisa mbalimbali walishirikishwa katika utafiti huu. Wahubiri hao walihitajika kujaza hojaji na vilevile kushiriki kwenye mahojiano ya ana kwa ana wakati wa kukusanya data. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa hoja zilizoathiri uteuzi wa lugha katika mahubiri ya Kikristo jijini Nairobi ni pamoja na: aina ya washiriki katika mazungumzo, muktadha wa mazungumzo, yaliyomo kwenye mazungumzo, uamilifu wa mazungumzo na malengo ya mazungumzo. Aidha, tuligundua kuwa wahubiri wa Kikristo jijini Nairobi waliteua lugha ya kutumia katika mahubiri wakizingatia jukumu mahususi ambalo lingetekelezwa na lugha iliyoteuliwa kufanikisha malengo yao ya Kimawasiliano. Utafiti unabainisha umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika kufanikisha mawasiliano ya kidini katika maeneo yaliyo na sifa ya wingilugha.
URI: https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/204/181
http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/8286
Appears in Collections:School of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
There are no files associated with this item.


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.