Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/8280
Title: Udhihirikaji wa mtafsiri katika muktadha wa baadaukoloni
Authors: Magugu, Vincent N.
Oduori, Robert W.
Kandagor, Mosol
Keywords: Uibuaji ugeni
Tafsiri za baadaukoloni
Issue Date: 2022
Publisher: Royallite publishers global
Abstract: Maendeleo katika taaluma ya tafsiri mwanzoni mwa miaka ya tisini yalibadilisha mtazamo kuhusu dhana ya tafsiri na kutambua upana na mabadiliko yake. Kupanuka kwa upeo wa taaluma hii kumeeleza na kuumba upya dhima ya mtafsiri. Nafasi ya mtafsiri imebadilika kutoka kwa daraja la kuvusha ujumbe pasi kuuathiri hadi kumtambua mtafsiri kuwa kiungo muhimu kinachoathiri mchakato na zao la tafsiri. Dhana kama vile ulinganifu, uaminifu pamoja na uhakiki wa ubora ambazo awali zilikuwa zenye umuhimu mkuu katika taaluma ya tafsiri zimesukumwa pembeni huku vipengele visivyokuwa vya kiisimu vikitiliwa mkazo. Ufasili na utafsiri wa matini ambao awali ulikuwa mchakato wa kiisimu na kimatini umebadilika na kujiegemeza zaidi kwa vipengele vya kitamaduni na vipengele nje ya isimu. Hali hii ni kweli tunapodhukuru tafsiri za fasihi katika muktadha wa baadaukoloni. Mtafsiri anadhihirika bayana kupitia kwa uteuzi wa kimakusudi ambao unajiegemeza kwa mikakati ya uibuaji ugeni hasa katika kushughulikia vipengele vinavyofungamana na utamaduni chanzi. Mikakati hii inaibua lugha mesto ambayo inahusiana kwa karibu na dhana ya utofauti wa kiisimu na kitamaduni katika mazingira ya baadaukoloni. Kwa kuchunguza tafsiri ya riwaya ya Caitaani Mutharaba-ini ya Ngugi wa Thiong’o kwa Kiingereza, Makala hii imejadili jinsi matini tafsiri imegeuzwa kuwa jukwaa la kukabiliana na ubabe wa kibepari katika ngazi ya isimu na utamaduni pamoja na jinsi udhihirikaji wa mtafsiri unavyobainika kupitia kwa kuchunguza uteuzi wa kimakusudi wa kiisimu ambao mtafsiri alifanya.
URI: https://www.royalliteglobal.com/african-languages/article/view/744
http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/8280
Appears in Collections:School of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
There are no files associated with this item.


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.