Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/8279
Title: Mabadiliko ya kimaana katika methali za kijinsia: mifano kutoka jamii ya wanyankole
Authors: Arinaitwe, Annensia
Kandagor, Mosol
Wafula, Magdaline
Keywords: Jinsia
Kinyankole
Issue Date: 2023
Abstract: Makala hii inachunguza mabadiliko kimaana na kimatumizi katika methali za kijinsia katika jamii ya Wanyankole. Lengo kuu la makala hii ni kubainisha athari ya mabadiliko katika jamii kwa kujikita kwenye ufasiri wa maana na matumizi ya methali za kijinsia miongoni mwa Wanyankole nchini Uganda. Mbinu za mahojiano zilitumika katika ukusanyaji wa data. Utafiti huu ulihusisha methali kumi na tano za kijinsia katika jamii ya Wanyankole. Uteuzi huo ulifanyika kimaksudi kwa kuwa utafiti ulilenga kuchanganua methali zilizohusu jinsia za kike na kiume katika jamii ya Wanyankole. Nadharia ya Udenguzi ilitumika katika uchanganuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kuwa kadri ulimwengu unavyobadilika ndivyo jamii ya Wanyankole inavyobadilika. Hivyo basi mabadiliko haya yameathiri ufasiri wa maana na matumizi katika methali za kijinsia za Wanyankole. Makala hii inapendekeza kuwa baadhi ya methali zinafaa kuchunguzwa upya kiufasiri, kimuundo na kimatumizi ili uamilifu wake uwiane na jamii ya kisasa.
URI: https://doi.org/10.58721/jkal.v1i1.94
http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/8279
Appears in Collections:School of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
There are no files associated with this item.


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.