Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/788
Title: ukiushi katika tafsiri: uhakiki wa tamthilia nitaolewa nikipenda
Authors: Kamotho John Njoroge
Keywords: NITAOLEWA NIKIPENDA
Issue Date: 12-Jan-2017
Publisher: MOI UNIVERSITY
Abstract: Utafiti huu umehusisha uchunguzi wa usuli wa sanaa ya tafsiri. Utafiti umechanganua kipengele cha ukiushi katika tamthilia Nitaolewa Nikipenda ambayo ni tafsiri ya Kiswahili ya tamthilia Ngaahika Ndeenda. Utafiti huu umefanya uchanganuzi linganishi wa lugha iliyotumiwa katika Matini Chanzi ya Ngaahika Ndeenda iliyo katika lugha ya Gĩkũyũ na Matini Tafsiri ya Nitaolewa Nikipenda iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. Utafiti umelenga kuchunguza Matini Tafsiri ilivyokiuka kutoka Matini Chanzi. Utafiti umechunguza zaidi dhana kuwa Matini Tafsiri ni ‘kivuli tu’ cha Matini Chanzi na hivyo kuihukumu kama kazi sahihi au isiyo sahihi. Utafiti huu umetumia Nadharia ya Mawasiliano katika Tafsiri ya Nida ambayo ni nguzo ya kanuni na michakato muhimu katika zoezi la tafsiri. Vitabu vya wataalamu mbalimbali vinavyohusu Nadharia ya Tafsiri na ukiushi katika tafsiri vimesomwa na mawazo yao kunakiliwa. Ngaahika Ndeenda na Nitaolewa Nikipenda vimesomwa kwa makini na kulinganishwa kwa mujibu wa lugha iliyotumiwa kwa kutumia maana kama kaida. Utafiti huu umechanganua ukiushi katika Tamthilia Tafsiri ya Nitaolewa Nikipenda na vilevile kujadili aina za ukiushi katika Tamthilia hii. Aidha umbuji kama kiungo cha ukiushi katika Matini Tafsiri ulitathminiwa. Tasnifu hii umejikita katika Nadharia ya Mawasiliano katika Tafsiri ya Nida ambayo husisitiza mawasiliano mwafaka kati ya Matini Tafsiri na Hadhira Pokezi. Utafiti umefanywa kwa kuchambua vitabu vya wananadharia wa tafsiri mbali na kuchanganua maneno ya Matini Tafsiri kwa kuyalinganisha na maneno ya Matini Chanzi. Sampuli za maneno, sentensi na vishazi vimetambuliwa na kunakililiwa kwa utaratibu, kuonyesha vilivyowakilishwa katika Matini Chanzi ya Gĩkũyũ na chini yake vilivyohawilishwa katika Matini Tafsiri ya Kiswahili. Maneno, vishazi na sentensi hizi zimechanganuliwa kiulinganishi halafu mahitimisho kufanywa. Uchanganuzi wa data iliyoshughulikiwa umethibitisha kuweko kwa ukiushi katika Matini Tafsiri. Ukiushi wowote uliopatikana katika Matini Tafsiri umeainishwa katika aina mbalimbali za ukiushi mathalani ukiushi wa kifonolojia, ukiushi wa kisintaksia na ukiushi wa kisemantiki. Athari ya maana ya ujumbe katika Matini Chanzi na Matini Pokezi imechunguzwa pia. Utafiti umezingatia dhima ya mtafsiri kama msanii na jinsi anavyokiuka maana iliyoko katika Matini Chanzi wakati anapotafsiri. Ni matumaini yangu kuwa utafiti huu utawafaa wanafunzi na wasomi ambao watatafitia mbinu za tafsiri katika kazi za kifasihi.
URI: http://ir.mu.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/788
Appears in Collections:School of Education

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Kamotho NKR 17 Finale pdf.pdf595.79 kBAdobe PDFThumbnail
View/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.