Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/7869
Full metadata record
DC FieldValueLanguage
dc.contributor.authorCherono, Naomi J.-
dc.contributor.authorMunyua, J. G.-
dc.contributor.authorOgechi, N. O.-
dc.date.accessioned2023-07-24T08:34:07Z-
dc.date.available2023-07-24T08:34:07Z-
dc.date.issued2019-
dc.identifier.urihttp://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/7869-
dc.description.abstractKila lugha ni mfumo huru unaojitosheleza kisarufi. Ingawa hivyo, wasemaji wa lugha tofauti wanapotagusana kimawasiliano, lugha zao huweza kuathiriana kisarufi, na athari mojawapo huwa ni ukopaji wa msamiati. Ni kutokana na hali hii ambapo utafiti huu ulichunguza kanuni zinazofuatwa katika uingizwaji wa msamiati mkopo wa Kiswahili na Kiingereza katika Kikipsigis. Makala hii ilichunguza mabadiliko ya kimofofonemiki yanayotokea katika msamiati mkopo unapoingizwa katika mfumo wa Kikipsigis. Vilevile, sababu za ukopaji zilibainishwa. Data ya utafiti iliteuliwa kimakusudi. Utafiti ulitambua kuwa Kikipsigis hufupisha irabu ndefu katika msamiati mkopo. Vilevile, irabu unganifu husahilishwa ili zikubalike katika Kikipsigis. Kimsingi tulitambua kuwa Kikipsigis hutohoa irabu ngeni kwa kutumia irabu asili zinazokaribiana kimatamshi. Ilibainika pia kwamba Kikipsigis hakiruhusu mfuatano wa konsonanti mwanzoni mwa neno. Kwa hivyo, Kikipsigis hutohoa msamiati wa aina hii kwa kuchopeka irabu. Katika kuchunguza vichocheo vya ukopaji, makala hii ilibainisha kwamba Kikipsigis hukopa msamiati ili kurejelea dhana ngeni isiyokuwepo katika utamaduni wake. Hata hivyo, uchanganuzi ulionyesha kuwa Kikipsigis wakati mwingine hukopa msamiati hata kama kina msamiati asilia kwa sababu ya ubadilishaji msimbo, msamiati mkopo ni sahili na rahisi kutamkwa ukilinganishwa na kisawe chake cha Kikipsigis.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherMoi university pressen_US
dc.subjectMsamiati Mkopoen_US
dc.subjectUtohozien_US
dc.subjectMabadiliko ya Kimofofonemikien_US
dc.titleMABADILIKO YA KIMOFOFONEMIKI KATIKA MSAMIATI MKOPO WA KIKIPSIGISen_US
dc.typeArticleen_US
Appears in Collections:School of Education

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
mabadiliko.pdf619.6 kBAdobe PDFView/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.