Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/7868
Title: UJASIRIAMALI WA KISWAHILI NCHINI KENYA
Authors: Cherono, N. Jesca
Ogechi, N. Oyori
Keywords: Ujasiriamali
Viswahili
Issue Date: 2018
Publisher: Moi university press
Abstract: Makala hii inatathmini shughuli za kiujasiriamali nchini Kenya kwa kutumia ‘Kiswahili’. Shughuli zinazoangaziwa zinajikita katika maeneo mbalimbali ambamo aina fulani za Kiswahili zinajitokeza kwa kuzingatia kwamba kuna “viswahili” vingi vinavyotumiwa nchini Kenya. Neno viswahili katika muktadha huu linatumika kwa maana ya aina mbalimbali za Kiswahili zisizo sanifu ambazo zinapatikana katika shughuli za kila siku zinazoendeshwa na binadamu. Viswahili hivi hutokana na wazungumzaji kutoka makabila na maeneo mbalimbali nchini Kenya wanaokitumia Kiswahili. Tumeendesha mjadala unaojaribu kuonyesha jinsi gani ujasiriamali wa Kiswahili umechangia katika kukua kwa Kiswahili katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini iliyopita. Mjadala huu umeongozwa na dhana ya ujasiriamali kama inavyofasiriwa na taaluma ya uchumi kwa kuiegemeza katika muktadha wa uchumi na lugha. Kwa hivyo, tumeangazia ujasiriamali katika shughuli mbalimbali kama vile vyombo vya habari, biashara kupitia mabango na uchapishaji. Isitoshe, tathmini imefanywa ili kudhihirisha athari chanya na hasi kisarufi na kimawasiliano katika kukua kwa Kiswahili kutokana na matumizi yake kiujasiriamali ili kufichua msambao wa athari hizo kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki
URI: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/7868
Appears in Collections:School of Education

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Makala ujasiriamali wa Kiswahili pdf 1.pdf741.28 kBAdobe PDFView/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.