Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/720
Title: kanga kama sajili maalum ya kisanii na mawasiliano
Authors: WACHARO, WACHARO JULIA
Keywords: MAWASILIANO
Issue Date: 12-Jan-2013
Publisher: MOI UNIVERSITY
Abstract: Istilahi mawasiliano ni tafsiri ya neno la Kiingereza „Communication‟ ambalo lina asili ya Kilatini „Com-uni-care‟ linalomaanisha kujadiliana au kuwa na mazungumzo. Mawasiliano ni mchakato ambao kwao habari hupokezwa baina ya mtu na mtu kupitia kwa mfumo ulio sawa wa alama au matamshi au ishara. Mara nyingi, mawasiliano haya huzua hisia kama furaha, huzuni, mapenzi na matumaini. Nyenzo mojawapo ya mawasiliano miongoni mwa wapwani wa Kenya ni kupitia kwa Kanga. Kanga ni kitambaa kipana chenye urefu wa sentimita 150 na upana wa sentimita 110 ambacho kwa kawaida huwa na maandishi ambayo hutumiwa kuwasilisha ujumbe fulani. Kanga hununuliwa na kuvaliwa mbili mbili (gora). Utafiti huu unafafanua uamilifu wa Kanga miongoni mwa wapwani wa Kenya kwa kuchunguza vazi hili kama makala maalum ya kusomeka. Utafiti wetu umeongozwa na nadharia mbili: Nadharia ya simiotiki iliyoasisiwa na Ferdinand de Saussure (1857 -1913), Charles Pierce (1839 -1914) na Roland Barthes (1915 - 1980) wanaosisitiza kuwa kila ishara huwakilisha ujumbe fulani. Nadharia ya uamali inayosisitiza kuwa muktadha ni kipengele muhimu katika mawasiliano. Tumeibua data kwa kushirikiana na wanajamii katika shughuli zao za kila siku huku tukiwasaili kuhusu Kanga na matumizi yake. Aidha, tumewatembelea wauzaji na watengenezaji Kanga ili watupatie data kuhusu mikondo inayotumiwa na wanunuzi wa kanga. Isitoshe, tumesoma maandishi ya wasomi tofauti hasa yale yanayohusiana na mada yetu. Mbali na hayo, tumepata ushauri kutoka kwa wataalam waliofanya utafiti kuhusu kanga wakiwemo Sheikh Nabhany (shairi „Utendi wa Ulimwengu wa Kanga‟) Marie Beck (Ambiguous Communication, kanga/leso) na Clarrisa Vierke. Mawasiliano yetu yalikuwa ya njia ya simu, intaneti na ana kwa ana. Sampuli iliyotumiwa imeteuliwa bila utaratibu maalum. Sura ya kwanza inatoa utangulizi wa tasnifu hii ilhali sura ya pili inaelezea historia na dhima zingine za kanga. Sura ya tatu inafafanua mawasiliano kupitia kwa kanga huku sura ya nne ikijikita katika kuchunguza uhusiano baina ya muktadha mnamotokea mawasiliano na mawasiliano mahsusi. Sura ya tano inatamatisha utafiti huu kwa kutoa mapendekezo.
URI: http://ir.mu.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/720
Appears in Collections:School of Education

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
WACHARO'S TASNIFU 2013 edited to the end.pdf2.51 MBAdobe PDFThumbnail
View/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.