Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/4434
Full metadata record
DC FieldValueLanguage
dc.contributor.authorKandagor, Mosol-
dc.contributor.authorJepkoech Singoei, Jane-
dc.contributor.authorMwanakombo, Mohamed-
dc.date.accessioned2021-05-12T07:45:14Z-
dc.date.available2021-05-12T07:45:14Z-
dc.date.issued2020-09-30-
dc.identifier.urihttp://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/4434-
dc.description.abstractUtafiti huu ulidhamiria kuchunguza jinsi vipengele vya kitamaduni katika matini teule ya Kiswahili na Kikalenjin vilivyochangia mtafsiri kuiandika upya Bukuit ne Tilil. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ambazo ni nadharia ya tafsiri vitendo ambayo ilitumika kubaini jinsi tofauti za kimazingira kati ya hadhira ya matini asilia na ya matini pokezi ilivyopelekea uandishi upya kufanyika wakati wa kutafsiri. Nadharia ya pili ni ya ulinganifu, ambapo matini asilia ililinganishwa na matini pokezi ili kubaini kama ujumbe ulihifadhiwa katika matini tafsiri. Aidha, tamaduni, matumizi ya msamiati na sarufi zililinganishwa kwa kuchunguza mikakati na mbinu zilizotumika kutafsiri matini asilia, na hivyo kubaini uandishi upya katika matini pokezi. Data zilikusanywa kupitia uchunguzi maktabani na vilevile kuwasaili washikadau katika Ofisi ya Utafsiri wa Bibilia ya Kapsabet na Shirika la Kutafsiri Biblia nchini, pamoja na wazungumza lugha ya Kikalenjin ambao walituelekeza juu ya matumizi ya baadhi ya maneno. Usampuli wa kimakusudi ulitumiwa ili kupata data iliyotumika katika uchanganuzi. Kitabu cha Mithali katika Agano la Kale kiliteuliwa kwa minajili ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa: utamaduni wa Waswahili na wa Wakalenjin ni tofauti na hii ilipelekea uandishi upya ufanywe katika tafsiri. Utafiti unapendekeza yafuatayo: Sera za elimu kuhusu lugha za kienyeji zinafaa kutilia maanani tafsiri ya matini za kufundishia.en_US
dc.publisherConsortium Publishingen_US
dc.subjectkitamadunien_US
dc.subjectmatinien_US
dc.subjectmtafsirien_US
dc.subjectBukuit ne Tililen_US
dc.titleJinsi vipengele vya kitamaduni katika matini teule ya kiswahili na kikalenjin vilivyochangia mtafsiri kuiandika upya Bukuit ne tilil.en_US
dc.typeArticleen_US
Appears in Collections:School of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Jane Jepkoech Singoei et al..pdf529.84 kBAdobe PDFView/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.