Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/4433
Title: Namna matumizi ya mikakati ya kutafsiri, kama uteuzi na mpangilio wa maneno, ilivyochangia katika uandishi upya wa Bukuit Ne Tilil.
Authors: Jepkoech Singoei, Jane
Kandagor, Mosol
Mwanakombo, Mohamed
Keywords: kutafsiri
uteuzi
mtafsiri
Bukuit ne Tilil
Issue Date: 30-Sep-2020
Publisher: Editon Consortium Publishing
Abstract: Utafiti huu ulidhamiria Kupambanua namna matumizi ya mikakati ya kutafsiri, ilivyochangia katika uandishi upya wa Bukuit Ne Tilil. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ambazo ni nadharia ya tafsiri vitendo ambayo ilitumika kubaini jinsi tofauti za kimazingira kati ya hadhira ya matini asilia na ya matini pokezi ilivyopelekea uandishi upya kufanyika wakati wa kutafsiri. Nadharia ya pili ni ya ulinganifu, ambapo matini asilia ililinganishwa na matini pokezi ili kubaini kama ujumbe ulihifadhiwa katika matini tafsiri. Aidha, tamaduni, matumizi ya msamiati na sarufi zililinganishwa kwa kuchunguza mikakati na mbinu zilizotumika kutafsiri matini asilia, na hivyo kubaini uandishi upya katika matini pokezi. Data zilikusanywa kupitia uchunguzi maktabani na vilevile kuwasaili washikadau katika Ofisi ya Utafsiri wa Bibilia ya Kapsabet na Shirika la Kutafsiri Biblia nchini, pamoja na wazungumza lugha ya Kikalenjin ambao walituelekeza juu ya matumizi ya baadhi ya maneno. Usampuli wa kimakusudi ulitumiwa ili kupata data iliyotumika katika uchanganuzi. Kitabu cha Mithali katika Agano la Kale kiliteuliwa kwa minajili ya utafiti huu. Utafiti huu ulibaini kuwa matumizi ya mikakati ya kutafsiri ilichangia uandishi upya wa kazi tafsiri. Uchunguzi huu ulipendekeza kuwa mashirika ya kufanya tafsiri yaimarishwe kwa kupewa uthamini ili kutafsiri makala nyingi Zaidi.
URI: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/4433
Appears in Collections:School of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Mosol Kandagor et al..pdf548.38 kBAdobe PDFView/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.