Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/4418
Title: Uongozi unavyojitokeza katika Fasihi ya Kisasa: Uchunguzi wa Riwaya Mpya ya Miaka ya 2000
Authors: Njenga, Alice Wanjiru
Keywords: Uongozi
fasihi
Riwaya
Issue Date: 2021
Publisher: Moi University
Abstract: Uongozi ni dhana muhimu sana katika jamii. Jamii zote ulimwenguni huwa na kiongozi wa aina fulani ambaye hutwikwa majukumu ya kuhakikisha kuwa watu wote walio chini yake wanapokea usawa kutokana na uongozi wake. Swala la uongozi limeshughulikiwa katika kazi za fasihi kwa namna tofauti tofauti. Utafiti huu uliangazia taswira ya uongozi inavyojitokeza katika fasihi ya kisasa kwa kuchunguza riwaya mpya za miaka ya 2000. Uliangazia mwelekeo mpya ambao unakisiwa umechukuliwa na baadhi ya waandishi wa riwaya mpya wanaoliona suala hili kwa mtazamo wa ndani nje. Madhumuni yafuatayo yalizingatiwa: Kufafanua taswira ya uongozi kama inavyosawiriwa na riwaya mbili mpya kwa kuangazia matatizo ya uongozi katika asasi za siasa na dini; Kutathmini mchango wa wananchi katika uongozi kwa mujibu wa riwaya zilizoteuliwa; na kuchunguza mtazamo wa ndani nje na mapendekezo yanayotolewa na riwaya kukabiliana na changamoto za uongozi. Riwaya za Msimu wa Vipepeo Wamitila (2007) na Paradiso Habwe (2010) ziliteuliwa. Data ilikusanywa kupitia usomaji makini wa riwaya zilizoteuliwa kwa kuzingatia mawazo ya waandishi yawe hasi au chanya kuhusu uongozi kwa kutumia uchambuzi wa yaliyomo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhistoria mpya. Data ilipangwa na kuchanganuliwa kimaelezo hivi kwamba mada zinazohusiana ziliwekwa na kuhusishwa kwa kijumla kama maoni ya waandishi kuhusu uongozi katika kipindi hiki maalum cha kihistoria. Utafiti huu umegundua kuwa uongozi bado ni changamoto katika asasi tofauti za kijamii na hasa katika siasa, serikali na dini ambazo zilishughulikiwa na riwaya zilizoteuliwa. Uongozi una athari za moja kwa moja katika maendeleo ya jamii na kwamba watawaliwa wanachangia tatizo hili. Waandishi wameonyesha kuwa ni lazima viongozi wayaangazie matatizo ya jamii kwa kushauriana na jamii badala ya kujiangazia wao binafsi. Pia, wananchi lazima wahakikishe kuwa viongozi wanawajibika kwa kujihusisha na masuala ya uongozi nchini. Katika dini, waandishi wanataka asasi hiyo iweze kujirekebisha kwa kuangazia maadili ya kidini ili jamii iwachukulie kwa dhati.
URI: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/4418
Appears in Collections:School of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Njenga Alice Wanjiru.pdf752.21 kBAdobe PDFView/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.