Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/3725
Title: Mwanga wa Lugha
Authors: Kandagor, Mosol
Keywords: Lugha
Issue Date: 2019
Publisher: Moi University Press
Abstract: Toleo hili linajumuisha jumla ya makala ambayo yanatanda katika taaluma mbalimbali za lugha na fasihi. Makala ya Tirus Mutwiri Gichuru, Kitula King’ei na Ireri Mbaabu yamebainisha kuwa maarifa na tajriba zilizofichamwa kwenye utambuzi huwa nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko ya maana za leksia. Imebainika wazi kuwa muundo wa maana na maumbile ya mwanadamu hasa hisia zake tano na ufasili wake wa ulimwengu husaidia mwanadamu kukabiliana na dhana mpya zinazoibuka katika mazingira halisi na ya kidhahania. Nao Amiri Swaleh and Rayya Timammy wamechambua utendi wa Mtu ni Utu (1978) uliotungwa na Ahmad Nassir Juma Bhalo. Waandishi wameangazia mafunzo makuu yanayojitokeza katika utendi huu; mafunzo ambayo yanakuza maadili ya kijamii. Uchambuzi huu umeegemea misingi ya Dini ya Kiislamu, kulingana na tajriba na maarifa ya mtunzi wa utendi huu. Makala ya Gakuo J. Kariuki yanaangazia baadhi ya changamoto zinazokumba taaluma ya ufasiri, uelewekaji na ufundishaji wa somo la ushairi katika shule za sekondari nchini Kenya. Mawazo na kauli zinazoshereheshewa katika makala haya zinazotokana na utafiti wa kisayansi uliofanywa katika kaunti mbili za Mombasa na Trans Nzoia. Rufus Karani Munyua, P. I. Iribemwangi na Tom M. Olali wameshughulikia suala la utafsiri kwa kudai kwamba chochote kinachoweza kusemwa katika lugha moja kinaweza pia kusemwa katika lugha nyingine. Waandishi hawa wamewarejelea wataalamu waliotukuka katika taaluma ya tafsiri kama vile Catford, Nida na Newmark kuhusiana na masuala wanayoyaibua.
URI: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/3725
Appears in Collections:School of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Mwanga wa Lugha.pdf1.07 MBAdobe PDFThumbnail
View/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.