Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/2472
Title: Uhakiki linganishi wa fani katika tafsiri mintarafu ya mkaguzi mkuu wa serikali (mwakasaka, 1979) na mkaguzi wa serikali (madumulla, 1999)
Authors: Serem, Sophia Jeptoo
Keywords: Stylistic devices
Issue Date: Nov-2018
Publisher: Moi University
Abstract: Utafiti huu ulilenga kutambua tofauti za kitafsiri katika tamthilia zilizotafsiriwa za Mkaguzi Mkuu wa Serikali (MMS) (Mwakasaka, 1979) na Mkaguzi wa Serikali, (MS) (Madumulla, 1999). Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kuhakiki kiulinganishi mbinu za lugha katika MMS na MS kuchambua kiulinganishi uwasilishaji wa ujumbe katika MMS na MS, kuchanganua kiulinganishi uteuzi wa msamiati katika usawiri wa wahusika katika MMS na MS. Upeo wa utafiti huu ulijikita katika MMS na MS. utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Uamilifu katika tafsiri mtazamo wa kuhakiki matini uliopendekezwa na Reiss (1977). Mihimili mikuu ya mtazamo huu ni: utambuzi wa kuhakikisha kuwa, kuna utoshelevu wa kimaana, kisarufi na kimtindo katika lugha lengwa kwa minajili ya kuuwasilisha ujumbe kwa wapokeaji wake, Kaida za matumizi ya lugha na uelewa ya kwamba kwa ajili ya mawasiliano maana ya neno hurejelewa kwa kuhusishwa na maneno mengine yanayohusiana na mada au muktadha wa diskosi unayozungumziwa, na kwamba matini pokezi inatarajiwa kudhihirisha mguso sawa na ule unaojitokeza katika matini asilia. Sampuli ya kimaksudi ilitumika katika uteuzi wa Mkaguzi Mkuu wa Serikali na Mkakuzi wa Serikali kwa sababu ni tamthilia zilizotafsiriwa na zinalenga matini asilia moja. Katika utafiti huu tulichunguza maonyesho yote yanayopatikana katika matini pokezi zilizoteuliwa. Ukusanyaji wa data ya tasnifu hii ulifanywa kwa kuzisoma kihakikifu matini zilizoteuliwa, kisha kuchanganua kiulinganishi mbinu za lugha, uwasilishaji wa ujumbe na usawiri wa wahusika mintarafu ya malengo ya utafiti na kwa kuongozwa na nadharia ya Uamilifu katika Tafsiri, Kitengo cha kuhakiki Matini kilichopendekezwa na Reiss. Uwasilishaji wa data ulifanywa kiufafanuzi na matokeo ya uchunguzi huu yatachangia marejeleo yanayohusu tafsiri linganishi. Ilidhihirika kuwa, mbinu za lugha, ujumbe au taarifa zilizowasilishwa na tabia za wahusika ni sifa bainifu zisizoweza kupuuzwa katika tafsiri linganishi. Aidha ilibainika kwamba, kuna tofauti katika matumizi ya mbinu za lugha, uwasilishaji wa ujumbe na uchanganuzi wa wahusika katika MMS na MS. Mtafiti anapendekeza kuwa, watafiti wa baadaye katika nyanja ya tafsiri linganishi wanaweza kushughulikia vitabu vingine tofauti na vilivyoshughulikiwa katika utafiti huu vilivyotafsiriwa na vinalenga matini asilia moja, huenda wakaibuka na matokeo tofauti. Hivyo, watafsiri wanaweza kupata kichocheo cha kutafsiri tena kazi za fasihi ambazo tayari zilishatafsiriwa. Washikadau katika uundaji wa silabasi ya Kiswahili katika vyuo vikuu wanaweza kutilia maanani kipengele cha Nadharia ya Uhakiki wa Matini katika kozi za tafsiri ili kuwawezesha wanafunzi kuwasilisha kazi za tafsiri zinazofaa zaidi. Isitoshe, utafiti huu utachangia kuibuka kwa tafiti za kuhakiki kiulinganishi vitabu vya fasihi vilivyotafsiriwa na watafsiri tofauti. Zaidi, utafiti huu utawafaa wanafunzi na wataalamu wa tafsiri linganishi.
URI: http://ir.mu.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/2472
Appears in Collections:School of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Serem Sophia Jeptoo 2018.pdf1.16 MBAdobe PDFThumbnail
View/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.