Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/2379
Title: Mwingiliano tanzu katika modern taarabu-mipasho
Authors: Murimi, Jackline Njeri
Keywords: taarabu-mipasho
Mwingiliano tanzu
Muziki
Issue Date: Nov-2016
Publisher: Moi University
Abstract: Taarab ni muziki wenye umaarufu mkubwa katika Afrika Mashariki kwa zaidi ya karne moja. Muziki wa taarab umepata mabadiliko makubwa na kusababisha kuwepo kwa aina mbili kuu za Taarab: Taarab Asili na Modern Taarab.Utafiti huu ulihakiki mwingiliano tanzu katika Taarab-Mipasho. Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni pamoja na kujadili mwingiliano tanzu kama unavyojitokeza katika miainisho ya tanzu za fasihi simulizi, kuchanganua miktadha mbalimbali ya mwingiliano tanzu katika muziki wa Taarab ya Mipasho na kutathmini dhima ya mwingiliano tanzu katika muziki wa Taarab ya Mipasho. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya mwingilianomatini iliyoasisiwa na Julia Kristeva (1960) baada ya kuizua kutokana na nadharia ya Mikhail Bakhtin ya Usemezano. Kutokana na nadharia ya mwingilianomatini, mtafiti ameitumia kushughulikia mwingiliano tanzu katika Taarab-Mipasho. Nadharia ya umuundo ilishirikishwa ili kutoa mwelekeo zaidi kuhusu uanishaji wa tanzu za fasihi simulizi kama ilivyopendekezwa na Finnegan. Pia nadharia hii ilitumika katika kufafanulia uhuru na ubunifu wa mtunzi wa kuingiza vipengele vipya katika kazi. Utafiti huu ulichukua muundo wa kimaelezo. Ukusanyaji data ulihusisha usikilizaji, utazamaji na unukuzi daftarini wa nyimbo za Taarab ya Mipasho ili kupata mistari, vifungu vya maneno na stanza zilizobainisha mwingiliano tanzu. Sampuli ya utafiti ilikuwa nyimbo 32 za muziki wa Taarab ya Mipasho ambazo ziliteuliwa kumaksudi. Uchanganuzi na uwasilishaji wa data ulitolewa kwa njia ya maelezo ya kina yaliyohusisha udondoaji na ufafanuzi wa mistari, vifungu vya maneno na stanza zenye kudhihirisha mwingiliano tanzu kutoka kwa data asili. Matokeo ya utafiti yalibainisha udhaifu mkubwa katika mbinu zinazotumiwa kuainisha tanzu za fasihi simulizi. Aidha, mwingilianotanzu mkubwa ulibainika katika uwasilishaji wa muziki wa Modern Taarab ya Mipasho uliorejelewa. Muziki wa Mipasho ulitekeleza dhima ya kuelimisha, kuhifadhi utamaduni, kuburudisha pamoja na kudhihirisha upekee wa msanii miongoni mwa dhima nyingine. Utafiti huu unawachochea wahahakiki wengine wa fasihi simulizi katika kufanya uchunguzi zaidi katika mitindo mingine ya nyimbo za modern taarab kwa misingi ya nadharia mbalimbali za fasihi. Aidha, kutokana na utafiti huu, ilitarajiwa kuwa watafiti wataweza kulinganisha na kulinganua mitindo tofauti ya taarab. Hatimaye, mtafiti anapendekeza tafiti zaidi zifanywe ili miongoni mwa mengine, kusuluhisha mgogoro kuhusu taarab ya mipasho, uainishaji wa tanzu za fasihi simulizi na waandishi katika miainisho ya utanzu wa nyimbo uwezekano wa kujumuisha nyimbo za taarab miongoni mwa vipera vya utanzu wa nyimbo katika awamu zote za usomi na uhakiki wa fasihi simulizi kwani muziki wa taarab na hasa mipasho bado unahitaji utafiti zaidi.
URI: http://ir.mu.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/2379
Appears in Collections:School of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
MURIMI, Jackline Njeri.pdf627.18 kBAdobe PDFThumbnail
View/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.