Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/1705
Title: Ukandamizaji wa Jamii unavyodhihirika katika Uandishi wa Clara Momanyi na Sheila Ali Ryanga na Nyamweya Omari Samwe
Authors: Nyamweya Omari Samwel
Keywords: Jamii
Ukandamizaji
Issue Date: Aug-2018
Publisher: Moi University
Abstract: Waandishi wanawake wameonyeshwa kama wanaondika kuhusu unyanyasaji wa wanawake pekee hata ikiwa mawanda ya kazi yao ni mapana. Pia, watafiti wengi wameguzia swala la ukandamizaji wa wanawake bila kuzungumzia wanajamii wanaokandamizwa. Utafiti huu ulichunguza usawiri wa wanaokandamizwa katika jamii na wanajamii kulingana na jicho la mwanamke: yaani jinsi waandishi wanawake wanavyowasawiri. Katika kuuendeleza na kuuchanganua zaidi, nilitumia riwaya mbili zilizoandikwa na waandishi wanawake: Nakuruto (2009) iliyoandikwa na Clara Momanyi na Dago wa Munje (2008) iliyoandikwa na Sheila Ali Ryanga. Riwaya hizi ziliweka wazi jinsi wanawake wanavyowaumba waliotengwa na kukandamizwa miongoni mwa wanajamii. Utafiti huu umebainisha waliotengwa ni akina nani kwa minajili ya kuwatambua wanavyosawiriwa katika riwaya hizi na pia katika jamii. Nadharia ya Jinsia-Hakiki ilitumika kuongoza utafiti huu. Nadharia hii iliasisiwa na Elaine Showalter na ilitokana na nadharia ya ufeministi. Nadharia ya Jinsia-Hakiki inanuia kutofautisha waandishi wanawake na waandishi wanaume. Nadharia hii inadai kuwa waandishi wanawake hushughulikia mambo ya kijamii zaidi tofauti na yale yanayoshughulikiwa na waandishi wanaume. Carter, akichangia kuhusu mihimili ya nadharia hii, anasema kuwa waandishi wanawake huandika kuhusu mada ambazo zimeepukwa na waandishi wanaume. Aidha anasema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya waandishi wanaume na waandishi wanawake katika kiwango cha maudhui na hata jinsi ya kusawiri wahusika. Tumetumia nadharia hii katika kuangalia jinsi waandishi wa kike wanawasawiri waliotengwa katika jamii na jinsi wanawasuluhishia matatizo yanayowakumba. Utafiti huu si linganishi. Utafiti huu ulitumia sampuli ya kimaksudi katika kupata data ambayo tuliishughulikia kuuendeleza utafiti. Tumewasilisha data kwa njia ya maandishi. Pia utafiti huu umechanganua jinsi waandishi wanawake wanavyowasawiri wanajamii wanaokandamizwa katika kazi zao za kifasihi mintarafu waandishi Clara Momanyi na Sheila Ali Ryanga; wakiwa ni waandishi wa kutoka Kenya. Waandishi wanawake wamepanua masuala wanayoyashughulikia katika kazi zao za kifasihi. Wanajamii wanawake kwa wanaume wanakandamizwa japo kwa viwango tofauti. Utafiti huu utasaidia kuwaheshimu waliokandamizwa na jamii na pia utawafaa wanafunzi, wahadhiri na wahakiki wa fasihi kuelewa zaidi kuhakiki kazi za fasihi zilizoandikwa na waandishi wanawake. Utafiti zaidi unafaa kufanywa kwa kazi tofauti za waandishi wanawake wengine.
URI: http://ir.mu.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/1705
Appears in Collections:School of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Nyamweya Omari Samwel 2018693.81 kBAdobe PDFThumbnail
View/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.