Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/10249
Title: Uteuzi wa lugha na mikakati ya kimawasiliano katika mandhari ya lugha mjini Eldoret
Authors: Kuttuny, Serah N.
Keywords: Uteuzi wa lugha
mandhari ya lugha
mikakati
mawasiliano
Issue Date: 2025
Publisher: Moi University
Abstract: Utafiti huu ulichunguza matumizi ya lugha na mikakati ya mawasiliano katika mandhari ya lugha mjini Eldoret. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kubainisha maudhui mbali mbali na mzagao wao katika mabango,kutathmini kwendana kwa uteuzi wa lugha kwa matarajio ya hadhira lengwa na kuchunguza ufaafu wa vielelezo vya mabango kama mikakati ya kuwasilisha ujumbe kwa hadhira lengwa. Utafiti huu ulijikita katika madai ya nadharia ya lugha-tarajiwa na isiyotarajiwa, baadhi ya madai ya nadharia ya lugha-solo na lugha-bebwa na nadharia ya semiotiki. Data za utafiti huu zilikusanywa katika barabara mbili kuu zilizoteuliwa kimakusudi mjini Eldoret; barabara ya Oginga Odinga na barabara ya Uganda. Makundi manne ya vijana na wazee yalihojiwa na kurekodiwa katikati mwa mji wa Eldoret. Usampulishaji kusudio ulitumika. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha maudhui mbali mbali na mzagao wao; benki (9.79%), elimu (1.39%), vinywaji (17.48%), bima (1.39%), uganga (0.69%), ajira (0.69%), vyakula (6.99%), Kamari (0.69%), habari na mawalisiano (18.88%), fenicha (0.69%), kilimo (9.09%), uchukuzi (9.09%), michezo (0.69%), bidhaa jumla (14.68%), matibabu (2.79%) na kongamano (2.79%). Pia, tuligundua ruwaza nne za uteuzi wa lugha; Kiingereza (49.65%), ubadilishaji msimbo (32.86%), Kiswahili (14.68%) na Kinandi (2.69%). Hatimaye, utafiti huu ulibainisha kuwa, uteuzi wa ujozi lugha katika mabango hayakuendana na matarajio ya hadhira. Hata hivyo, utafiti huu uling`amua kuwa matumizi ya viziada lugha kama vile picha, rangi na fonti mbali mbali hushadidisha mawasiliano katika matangazo ya mabango. Tasnifu hii inapendekeza kuwa, kwa kuwa mandhari ya lugha mjini Eldoret yameonyesha ubadilishaji msimbo na lugha zisizo thabiti za Sheng na Engsh huku lugha ya asili ya eneo la mji wa Eldoret, Kinandi, ikitumika kwa uchache sana. Ukweli ni kwamba haiwezekani kujumlisha hali ya mandhari ya lugha nchini Kenya kwa kujikita katika mji mmoja tu. Kwa hivyo, tunapendekeza utafiti zaidi uendeshwe katika miji mingine.
URI: http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/10249
Appears in Collections:School of Arts and Social Sciences

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Kuttuny Serah N. pdf8.78 MBAdobe PDFView/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.